Visit our COVID-19 resource hub   

Ahadi yetu kuhusiana na usawa, utofauti, na ujumuishaji

Kwa muda mrefu sasa, Blue Ventures imekuwa ikijitahidi kufanya kazi zake kwa njia ambazo zinakabiliana na dhuluma za kijamii zinazoandamana na shughuli za uhifadhi, ambazo zimeshamiri katika historia ya hivi karibuni. Tunaamini kwamba kuimarisha Usawa, kuondoa tofautina, Ujumuishaji wa wadau wa jinsia, rika, na tamduni tafauti katika uhifadhi kutaondoa udhalimu huu, na pia utajenga harakati za uhifadhi zenye mafanikio zaidi, zikiongozwa na mashirika yenye ufanisi utokanao na timu za wafanyakazi wanaoakisi upana wa tamaduni na makundi ya kijamii na kijinsia pamoja na  na kuthamini uhuru wa jamii wanazotumikia.

Dhamira yetu ya asili, na maadili ya shirika letu vinasimamia kuimarisha nguvu na uwezo wa jamii katika kusimamia uhifadhi. . Licha ya kushikilia kwa karibu maadili haya katika shughuli zetu, tunakiri kwamba udhalimu na ukosefu wa usawa unaonekana kote katika kazi yetu, shirika letu na sekta yetu.

Mabadiliko tunayoyataka yanahitaji uwajibikaji, tafakuri, kuwa wakweli baina yetu na kati yetu na jamii tunazofanya kazi nazo, na vilevile kukubali ukweli mgumu pindi unapojitokeza. Tukiongozwa na sauti za Watu Weusi, Watu Asilia wa maeneo yao na watu Wenye Ngozi iliyo na Rangi (BIPOC) katika timu zetu, washirika wetu, na jamii tunazozohudumia, tunaahidi kushughulikia kikamilifu na kwa uwazi aina zote za ubaguzi – ikiwemo ubaguzi wa rangi uliopo katika mifumo – kwa kuanzia na shirika letu. Kwa kufanya hivyo, tunaendelea na safari yetu ya kuunga mkono harakati zilizo haki na jumuishi kwa uhifadhi wa bahari ambazo zinawakilisha uzoefu wa wavuvi wadogo na jamii za pwani duniani kote.

Mnamo mwezi wa tisa na kumi mwaka 2020, tuliwezesha baadhi ya majadiliano ya vikundi na kuwaalika wafanyakazi wenzetu watoe uzoefu wao kuhusiana na Usawa, Uanuwai, na Ujumuishaji ndani ya Blue Ventures. Zaidi ya wafanyikazi 160 (asilimia 60 ya timu yetu iliyopo katika nchi mbalimbali duniani) walichangia kwenye majadiliano hayo na tafiti za siri zilitumwa kwa wafanyakazi wote. Tunawashukuru wote waliotoa maoni yao, pamoja na uzoefu wao binafsi, na kuweka wazi njia nyingi ambazo tunaweza kutumia kuboresha ufanyaji wetu wa kazi kama shirika.

 

Baada ya timu yetu kutafakari, tunachukua hatua zifuatazo kuimarisha Usawa, na Ujumuishaji wa wadau wa rika, jinsia na mila fafauti katika Blue Ventures:

 • – Tumeunda jukwaa ndani ya mfumo wetu wa mawasiliano ya ndani ambapo wafanyakazi wenzetu wanahimizwa kuweka rasilimali, nakala, filamu na mawazo muhimu kuhusiana na suala la haki za kijamii na jinsi gani zinaingiliana na kazi zetu. Tunataka kuhakikisha kuwa jukwaa hili ni jumuishi na linaweza kufikiwa na wahusika wote kadri inavyowezekana, kwa hivyo tarajia kuwa uendeshaji wa jukwaa hili utabadilika na kukua kadri tunavyozidi kupokea maoni kutoka kwa wafanyakazi wenzetu.
 • – Hivi sasa tunahakikisha kuwa maombi yote ya kazi yanafanyika bila kuonyesha taarifa za mwomba kazi katika mchakato wa kuchuja maombi, na kwamba maelezo ya kazi hayaoneshi jinsia ya muombaji ili kuzuia upendeleo wa mhakiki. Vilevile tumeweka viunganishi kwenye mfumo wetu wa ufuatiliaji wa waomba kazi kwa ajili ya wafanyikazi wetu ambapo kuna video zinazotoa utangulizi juu ya suala la ubaguzi usiokusudiwa, utofauti, ujumuishaji, na zana za kusaidia kubainisha utangazaji wa ajira yenye maelezo ya kijinsia. Kanuni zetu za kuajiri zipo ndani ya sera yetu ya ajira na mojawapo ni kutobagua pamoja na kuweka msisitizo juu ya utofauti.
 • – Tumeanzisha Kikundi Kazi cha Usawa, Uanuwai na Ujumuishaji chenye jukumu la kukuza, kutetea na kuhamasisha masuala haya katika kazi zetu. Kikundi hiki kinawakilisha uanuwai wa timu yetu iliyopo nchi mbalimbali duniani. Timu hii ina wafanyakazi 15 wenye viwango tofauti vya ukongwe pamoja na angalau mwakilishi mmoja kutoka timu zetu tano za nchi.

 

Kikundi Kazi kinawajibika kwa yafuatayo:

 • – Kuzingatia masuala, mashaka, na mawazo mengine yaliyotolewa wakati wa majadiliano ya vikundi yaliyofanyika mwezi wa Septemba na Oktoba mwaka 2020.
 • – Kutambua vipaumbele vya Usawa, Utofauti na Ujumuishaji na kutambua mapungufu katika sera na taratibu zilizopo.
 • – Kuandaa mpango wa utekelezaji utakaokaguliwa na mshauri wa nje wa masuala ya Usawa, Utofuti , na Ujumuishaji mwishoni mwa mwaka fedha wa 2021.
 • – Kusaidia utekelezaji wa kazi za mpango wa Usawa, Utofauti, na Ujumuishaji.
 • – Kushiriki katika mafunzo yanayohusiana na Usawa, Utofauti , na Ujumuishaji, mfano ubagazi usiokusudiwa, dhana ya utofauti na ujumuishaji.
 • – Kutetea Usawa, Utofauti, na Ujumuishaji ndani ya shirika, na kulazimisha, wafanyakazi binafsi na vikundi vya uongozi kuunda mazingira yenye utamaduni wa usawa, utofauti na ujumuishi mahali pa kazi.
 • – Kufuatilia na kufanya mawasiliano na shirika zima juu ya takwimu za Usawa, Utafauti, na Ujumuishaji zilizokubaliwa na Kikundi Kazi cha Usawa, Utafauti, na Ujumuishaji.
 • – Kuiwakilisha Blue Ventures kwenye jamii katika mambo yanayohusiana na Usawa, Utofauti , na Ujumuishaji.

Tunashukuru kwamba tumeanza safari hii ndefu ya kuondokana na tabia zilizojengeka na mwenendo uliopo; tunaazimia kuwa wasikivu na kuendelea kuboresha uendeshaji wetu. Tunafanya kazi kikamilifu kuhakikisha kuwa usawa, utofauti, na ujumuishaji unakuwa ni jiwe la msingi la uhusiano wetu wa kitaalam, ndani ya Blue Ventures na katika ushirikiano na wadau wetu mbalimbali.

Pin It on Pinterest