Kongamano la Vijana lililofanyika mjini Stirling, lililenga kukuza nafasi ambayo vijana wanaweza kutekeleza katika nyanja ya maendeleo endelevu na kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa.
Zaidi ya wanaharakati vijana 600 walio na nguvu zaidi duniani katika nyanja ya maendeleo endelevu, kutoka zaidi ya nchi 120 tofauti, walihudhuria Kongamano kujadili masuala yanayohusu mabadiliko ya hali ya hewa, kupunguza umaskini, elimu, masuala ya jinsia, na Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Kongamano la Vijana Duniani huko Stirling tembelea: www.scotland2005.org . Taarifa kuhusu makongamano yajayo zinaweza kupatikana katika: http://www.peacechild.org





