Utafiti huo uliangalia imani za kidini, matumizi ya kihistoria ya rasilimali za baharini, shughuli za kila siku, utegemezi wa kiuchumi kwenye uvuvi, maarifa ya ndani ya mabadiliko ya mazingira pamoja na masuala mengine ya kitamaduni.
Taarifa hii ni muhimu kwa ajili ya kuandaa mikakati madhubuti ya uhifadhi ambayo itanufaisha jamii za wenyeji na rasilimali za baharini zilizo hatarini.
"Ili kufanya ulinzi wa miamba ya matumbawe kuwa na ufanisi katika jumuiya yenye maendeleo duni kama vile Andavadoaka ni muhimu kuelewa uhusiano kati ya rasilimali za baharini na watumiaji wake," alisema mwanasayansi wa masuala ya kijamii wa Blue Ventures Josephine Langley ambaye aliandika utafiti huo. "Kutambua njia za kuepuka mahitaji yanayoweza kugongana ya maendeleo ya kiuchumi na uhifadhi ni muhimu."
Miradi mingi ya uvuvi na usimamizi wa uhifadhi wa bahari duniani kote imeshindwa kwa sababu jumuiya za wenyeji zilitengwa katika mchakato wa uhifadhi.
Ushirikishwaji wa jamii, utafiti shirikishi na kukuza matumizi ya maarifa ya wenyeji vimejitokeza mara kwa mara kama hatua muhimu za kushughulikia tatizo la kusimamia maendeleo ya watu na uchumi wao na kulinda mazingira kwa wakati mmoja.
Ripoti inaweza kupakuliwa kwa http://blueventures.org/research/Langley_TEK_2006_(web).pdf