Matt Hudson, mwenye umri wa miaka 24, mfanyakazi wa kujitolea kwenye safari ya kwenda Andavadoaka, Madagaska mnamo Septemba 2008, alipiga picha wakati akifanya utafiti na shirika lisilo la kiserikali la Blue Ventures la uhifadhi wa baharini. Picha ni ya kaa mdogo wa porcelaini ambaye Matt alimwona akiwa amejificha kwenye anemone alipokuwa akichunguza mwamba.
Hii si mara ya kwanza kwa picha hiyo kushinda tuzo - pia ilishinda tuzo katika shindano lililoendeshwa na PADI Sports Diver magazine kwa ajili ya kupiga picha chini ya maji katika maji ya joto.
Nakala asili iliyowekwa kwenye Daily Telegraph's