Hivi majuzi DW ilichapisha kipande kuhusu athari za kupungua kwa hifadhi ya samaki na mabadiliko ya hali ya hewa katika jamii za pwani nchini Madagaska, na njia mbadala za kujikimu ambazo jumuiya hizi zinageukia huku uvuvi unapokuwa usio endelevu.
Huko Tampolove, kijiji kidogo kusini mwa Madagaska, ambapo chakula cha watu kinajumuisha samaki na mchele, wavuvi wameanza kilimo cha mwani.
Kwa usaidizi wa Blue Ventures , kikundi cha uhifadhi wa baharini chenye makao yake Uingereza, Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori , na Chuo Kikuu cha Toliara , kijiji kimeanza kukuza mwani kwa ajili ya soko la Ulaya.
Katika miaka michache iliyopita, jamii pia imeanza kujaribu kilimo cha matango ya baharini ( Holoturia scabra ), na moss wa baharini wa elkhorn ( Kappaphycus alvarezii ). Moss wa baharini ni aina ya mwani mwekundu, ambapo carrageenan - jeli inayotumika katika tasnia ya chakula na vipodozi - hutolewa.
Kilimo cha mwani kinaonekana kufanikiwa katika kijiji hicho; uzalishaji umepanda kutoka tani 13 mwaka 2013 hadi tani 187 mwaka 2016. "Na tunatarajia kufikia tani 250 mwaka huu," alisema kiongozi wa jumuiya Badouraly.
Soma makala kamili: Hakuna samaki tena? Tutafuga mwani badala yake
Soma kuhusu mnara mpya wa usalama unaowalinda wakulima wa matango ya baharini huko Tampolove.





